VIWANJANI | Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally ametangaza rasmi viingilio vya Derby ya Kariakoo, huku Mzunguko ikiwa ni Sh. 20,000 na VIP Sh. 50,000.
Ahmed amesema maandalizi yote ya kiufundi na kiutawala yamekamilika kuelekea mchezo huo wa Kariakoo Derby utakaopigwa Oktoba 10, 2026.
Aidha, Ahmed amezungumzia hali ya kikosi cha msimbazi kwa kusema ujasiri wa timu hiyo kuelekea mchezo wa Kariakoo Derby unatokana na ari ya wachezaji pamoja na matokeo mazuri waliyopata katika michezo ya hivi karibuni.
Ahmed amesema Derby hiyo itakuwa na nafasi ya kutoa majibu kuhusu uwezo na hali ya Simba SC kwa sasa.